VIENNA: Iran haitaepuka vikwazo vya baraza la usalama la umoja wa mataifa
22 Agosti 2007Mjumbe mkuu katika mazungumzo ya shirika la kimataifa linalodhibiti matumizi ya atomiki Gregory Schulte amesema kwamba utayarifu wa Iran katika kujibu maswali yanayohusu mpango wake wa nyuklia hayataiepushia nchi hiyo mpango wa kuwekewa vikwazo na baraza la usalama la umoja wa mataifa.
Bwana Schulte ametoa matamshi hayo baada ya taarifa kwamba Iran na shirika la kimataifa linalodhibiti matumizi ya atomiki zimefikia makubaliano ya kushughulikia maswali kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.
Awali naibu wa shirika hilo la kimataifa Olli Heinonen alieleza kwamba mazungumzo ya nyuklia yaliyofanyika mjini Tehran yalikuwa na mueleko mzuri.
Wakati huio huo rais Mahmoud Ahmednejad wa Iran amekamilisha ziara yake nchini Azerbaijan kwa kutamka kuwa nchi yake ina haki ya kuendeleza teknolojia ya nyuklia iliyo salama.