VIENNA: Iran itatafuta njia ya kusuluhisha mgogoro
23 Juni 2007Matangazo
Mkurugenzi wa Shirika la Nishati ya Atomu la Umoja wa Mataifa-IAEA-bwana Mohammed El-Baradei amesema,Iran ipo tayari kutafuta njia za kusuluhisha mgogoro unaohusika na mradi wake wa nyuklia.El-Baradei akaongezea kuwa ameridhika na majadiliano yake pamoja na mjumbe mkuu wa Iran,bwana Ali Larijani.
Amesema,ni matumaini yake kuwa katika kipindi cha majuma machache yajayo wataweza kutayarisha mpango wa hatua za kuchukuliwa. Anatumaini kuwa utaratibu huo utakamilishwa katika muda wa miezi miwili.