Vienna. Iran kufikishwa katika baraza la usalama.
19 Septemba 2005Matangazo
Mazungumzo yanatarajiwa kuanza baadaye leo mjini Vienna juu ya uwezekano wa kuipeleka Iran katika baraza la usalama la umoja wa mataifa kwa ajili ya kuwekewa vikwazo juu ya mpango wake wa kinuklia.
Wajumbe kutoka Ujerumani, Uingereza na Ufaransa tayari wanasemekana wanaufanyia kazi muswada wa azimio ambao utawasilishwa katika bodi ya magavana wa shirika la kimataifa la nishati ya Atomic kwa ajili ya uamuzi baadaye wiki hii.
Hii inakuja baada ya hotuba ya rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad katika baraza kuu la umoja wa mataifa mjini New York siku ya Jumamosi, ambapo amesisitiza kuwa Iran itaendelea na shughuli zake za kurutubisha madini ya Uranium.
Urutubishaji wa madini hayo ya Uranium kunaweza kutumika katika kutengeneza silaha za kinuklia.