1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIENNA: Mafuta kuongezwa:

20 Septemba 2005

Wawakilishi wa shirika la nchi zinazozalisha mafuta OPEC, wanaendelea na mkutano wao mjini Vienna ambapo wanajadili uwezekano wa kuongeza uzalishaji wa bidhaa hiyo.

Wawakilishi hao wanazungumzia juu ya kuongeza mapipa milioni moja kwa siku ili kuikabili hali iliyosababishwa na kimbunga Katrina nchini Marekani.

Lakini pia pana mawezekano ya kuzalishwa mapipa hadi milioni mbili kwa siku.

Uamuzi juu ya hayo unatarajiwa kufikiwa leo kwenye mkutano huo wa mjini Vienna.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW