VIENNA: Makubaliano hayajafikiwa kuhusu hali ya baadaye ya Kosovo
2 Machi 2007Matangazo
Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa, Marti Ahtasaari, amesema makubaliano hayajafikiwa katika mazungumzo kuhusu hali ya baadaye ya jimbo la Kosovo.
Ahtasaari amewaambia waandishi wa habari mjini Vienna Austria hii loe kwamba mazungumzo kati ya maafisa wa Serbia na Albania yamemalizika bila kufikia muafaka. Aidha kiongozi huyo amesema pande hizo mbili bado zinapinga mpango mpango wa Umoja wa Mataifa utakaofungua mlango kwa uhuru kwa Kosovo.
Jamii ya Walbania katika mkoa wa Kosovo wanahisi pendekezo hilo halitoia maelezo ya kina huku Serbia kwa upande wake ikisema haitakubali uhuru wa Kosovo.
Marti Ahtasaari amesema Waserbia na Walbania wana nafasi ya mwisho kumaliza tofauti zao katika duru ya mwisho ya mazungumzo wiki ijayo.