VIENNA : Mzozo wa nuklea wa Iran wadhibiti mkutano
10 Septemba 2007Matangazo
Mzozo wa nuklea kati ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Iran umekuwa ukihodhi mkutano wa nchi wanachama 35 wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomu.
Ali Larijani mjumbe wa Iran amesisitiza tena kwamba taifa hilo la Kiislamu litaendelea kurutubisha uranium iwapo baraza la usalama litaiwekea vikwazo zaidi nchi hiyo.
Kiongozi wa shirika hilo la nuklea la Umoja wa Mataifa Mohamed El Baradei amesema leo hii serikali ya Iran lazima ichukuwe hatua ziada ya mpango wenye kikomo kwa ajili ya kuziweka wazi shughuli zake za nuklea ili kwamba kuondowa hali ya kutoaminika kwa shughuli zake hizo.