VIENNA: Shirika la IAEA laikosoa Marekani
15 Septemba 2006Matangazo
Shirika la kimataifa la kuzuia uenezaji wa silaha za nyuklia, IAEA, limeilalamikia serikali ya Marekani juu ya ripoti ya uongo na kupotosha kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.
Barua ya shirika hilo imefichua kwamba ripoti ya bunge la Marekani kuhusu matokeo ya uchunguzi wake wa mpango wa nyuklia wa Iran, ilikuwa na habari za kupotosha.
Ripoti hiyo iliyotangazwa mwezi uliopita, inailaumu Iran kwa kujaribu kutengeneza silaha za nyuklia, ikitaja pia kukataa kwa Iran kusitisha kurutubisha madini ya uranium na ushahidi mwingine.
Shirika la IAEA pia limepinga habari za kuondolewa kwa afisa wa uchunguzi wa ngazi ya juu katika vinu vya nyuklia vya Iran. Kufikia sasa Marekani haijatoa matamshi yoyote kuhusu barua hiyo.