Vienna. Ujumbe wa IAEA kwenda Korea ya kaskazini.
9 Julai 2007Matangazo
Shirika la kimataifa la nishati ya Atomic limeidhinisha mipango ya kutuma kundi la wachunguzi nchini Korea ya kaskazini baadaye wiki hii ili kuangalia kazi ya kufunga kabisa mpango wa silaha za kinuklia wa nchi hiyo.
Mkuu wa shirika hilo la IAEA Mohammed El-Baradei amesema kuwa hii ni hatua muhimu kuelekea katika njia sahihi.
Hatua hiyo imeidhinishwa leo Jumatatu na bodi ya mataifa 35 wanachama wa shirika hilo, ambayo ilifanya kikao chake maalum leo mjini Vienna. Wanadiplomasia wanasema kuwa ujumbe huo utagharimu kiasi cha dola milioni 5 katika muda wa miaka miwili , na kwamba Marekani iko tayari kutoa kiasi kikubwa cha fedha hizo.