VIENNA : Umoja wa Ulaya yaahirisha kuifikisha Iran katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
22 Septemba 2005Matangazo
Wanadiplomasia wa Ulaya hapo jana wameamuwa kuahirisha shinikizo lao la kutaka kuifikisha Iran katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika kura ya bodi ya Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki kutokana na mpango wake nuklea.
Uamuzi huo inaonekana umefikiwa kutokana na wasi wasi wa kuwepo upinzani mkubwa kutoka zaidi ya nchi 12 miongoni mwa nchi 35 wanachama wa bodi ya IAEA wanaokutana mjini Vienna zikiwemo nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Russia na China.
IAEA imekua ikiichunguza Iran tokea mwezi wa Februari mwaka 2003 kwa madai kwamba serikali ya Tehran imekuwa ikitumia mpango wa nuklea wa shughuli za kiraia kwa ajili ya kuficha mpango wake wa kutengeneza silaha za nuklea.