VIENNA : Wakaguzi wa nuklea kuwepo Korea Kaskazini
10 Julai 2007Matangazo
Shirika la masuala ya nuklea la Umoja wa Mataifa limekubali kutuma wakaguzi wa nuklea nchini Korea Kaskazini kwa mara ya kwanza kabisa tokea mwaka 2002 kusimamia kufungwa kwa mtambo mkuu wa nuklea nchini humo.
China imesema inataka mazungumzo ya nuklea ya nchi hiyo yaanze tena wiki ijayo.Korea Kaskazini ilikubali kuufunga mtambo wale Yongbyon katika makubaliano ya pande sita yaliofikiwa mwezi wa Februari.
Makubaliano hayo ni hatua ya kwanza kwa serikali ya Korea Kaskazini kuachana na silaha zake za nuklea na badala yake kupatiwa msadaa wa nishati kutoka Korea Kusini.