VIENNA:Iran imeanza kuchuja mafuta ya kinyuklia yasema IAEA
19 Aprili 2007Matangazo
Shirika la kimataifa la udhibiti wa nishati ya nyuklia limethibitisha kuwa Iran imeanza kuchuja mafuta ya kinyuklia katika mtambo wake wa Natanz. Balozi mmoja amesema mjini Vienna kuwa wanasayansi wa Iran wameunganisha mapipa pewa, 1300 na kuyajaza gesi inayohitajika kwa ajili ya kurutubisha madini ya uranium.
Mapema wiki jana rais wa nchi hiyo bwana Ahmadinejad alitangaza kuwa nchi yake sasa ina uwezo wa kuzalisha madini hayo kwa kiwango kikubwa.
Iran inasisitiza kuwa mpango wake wa nyuklia ni wa kuzalisha nishati kwa matumizi ya amani lakini nchi za magharibi zinahofia kuwa nchi hiyo inakusudia kuunda silaha za kiatomiki.