1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIENNA:Mazungumzo na Iran yaendelea vizuri wasema Umoja wa Ulaya

10 Septemba 2006

Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya bwana Havier Solana amekutana na mjumbe wa Iran bwana Ali Larijani kuzungumzia mzozo wa nyuklia wa nchi hiyo , mjini Vienna.

Msemaji wa Umoja wa Ulaya amearifu kuwa mazungumzo hayo yameendelea vizuri. Bwana Solana na mjumbe huyo wa Iran wanatarajiwa kukutana tena leo ili kuangalia uwezekano wa kuanzisha tena mazungumzo rasmi juu ya pendekezo lililotolewa na nchi tano , wanachama wa kudumu wa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Ujerumani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW