Vietnam yakamata kilo 500 za pembe za ndovu
2 Desemba 2016Matangazo
Afisa wa forodha katika mji wa Ho Chi Minh, Pham Quang Nam, ameliambia shirika la habari la Ujerumani (dpa) kwamba maafisa walipewa taarifa kutoka duru za kimataifa kabla ya kuwakamata wahalifu hao.
Walanguzi wa biashara ya pembe za ndovu mara nyingi huficha pembe katikati ya mbao, lakini matumizi ya kifaa maluum cha ukaguzi wa mbao kinawasaidia maafisa wa forodha kuzikamata pembe hizo.
Walanguzi hao hutumia sana nchi ya Vietnam kama kituo cha kupitishia mzigo wao unaokwendea China.