1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMamlaka ya Palestina

Vifaru na ndege za Israel vyazidisha madhila Gaza

18 Septemba 2025

Magari ya kivita na ndege za kijeshi za Israel zimeshambulia mji wa Gaza City kwa nguvu kubwa leo Alhamisi, na kusababisha maelfu ya raia wa Palestina kukimbia kwa hofu wakiwa na mizigo yao.

Ukanda wa Gaza.
WHO, imeonya kuwa maagizo ya kuhamia kusini yaliyotolewa na jeshi la Israel yamesababisha wimbi jipya la wakimbizi wa ndani.Picha: Eyad Baba/AFP/Getty Images

Mashuhuda wanasema mashambulizi ya mizinga na mabomu hayajakoma, huku familia zikilia na kuomboleza barabarani.

Shirika la Afya Duniani, WHO, limeonya kuwa maagizo ya kuhamia kusini yaliyotolewa na jeshi la Israel yamesababisha wimbi jipya la wakimbizi wa ndani, wakati hospitali zikiwa ukingoni mwa kuporomoka.

Hospitali ya Al-Shifa imeripoti kupokea miili ya watu 20 waliouawa tangu usiku wa manane, huku zaidi ya watu 60 wakipoteza maisha kwa siku moja.

Jeshi la Israel linadai kuzilenga ngome za Hamas, lakini ghadhabu ya kimataifa inaongezeka baada ya Umoja wa Mataifa kuituhumu Israel kwa mauaji ya kimbari.

Wakati huo huo, familia za mateka wa Kiisraeli walioko Gaza zilifanya maandamano mjini Jerusalem, wakimtuhumu Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kwa kushindwa kuwaokoa wapendwa wao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW