1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vifaru vya kijeshi vya Israel vyaendeleza mashambulizi Rafah

29 Mei 2024

Vifaru vya Israel vimeendelea kushambulia katika mji wa Rafah kwa siku ya pili leo na kukaidi uamuzi uliotolewa na mahakama ya Kimataifa ulioitaka nchi hiyo isitishe hatua ya kuushambulia mji huo wa Kusini mwa Gaza.

Israel
Vifaru vya kijeshi vya Israel vyaendeleza mashambulizi RafahPicha: Leo Correa/AP Photo/picture alliance

Israel imeendeleza mashambulizi hayo leo baada ya Marekani kusema hatua zinazochukuliwa na Israel hazijafikia operesheni kubwa za kijeshi katika mji huo.Marekani iliitahadharisha Israel kuepuka kufanya mashambulizi makubwa.

Jana ni mara ya kwanza Israel kupeleka vifaru katikati ya mji wa Rafah  licha ya mahakama ya Kimataifa inayosimamia haki,iliyoko nchini Uholanzi kuitaka isitishe mashambulizi kwenye mji huo.

Israel kuendeleza vita Gaza hadi mwishoni mwa mwaka 2024

Wakaazi wa Rafah wamesema vifaru hivyo vya kijeshi vya Israel viliingia hadi magharibi mwa mji huo kabla ya kuelekea kwenye eneo la usalama lililowekwa  lililoko katika mpaka na Misri.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW