1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vifo 42 katika shambulio huko Urusi ya Kusini:

6 Desemba 2003
MOSKO: Siku moja baada ya kushambuliwa treni ya abiria
huko Urusi ya Kusini, vikosi vya usalama
vimegundua bomu jengine katika treni ya mizigo.
Shirika la Habari la Urusi, ITAR-TASS limearifu
kuwa bomu hilo lilifichwa katika mojawapo ya
magurudumu ya treni hiyo. Watu 41, na siyo 42,
wameuawa iliposhambuliwa treni ya abiria hapo
jana. Zaidi ya watu 200 wamejeruhiwa. Rais
Vladimir Putin ameshutumu kuwa shambulio hilo
lilifanywa kama jaribio la kueneza wasi wasi
muda mfupi kabla ya kuanza uchaguzi wa bunge.
Kwa kufuatana na taftishi za hadi sasa,
inasemekana ni magaidi wa Kichechenia
waliojitolea mhanga maisha waliyoishambulia
treni hiyo ya abiria katika mji wa Yessentuki.
Mkuu wa waasi wa Kichechenia, Aslan Mashadow
amepinga shutuma zozote za kuhusishwa kwake na
shambulio hilo. Shambulio hilo limelaumiwa
vikali kimataifa. Mbali na Rais wa Halmashauri
ya UU, Romano Prodi, naye Katibu Mkuu wa UM,
Kofi Annan amewapelekea risala za rambi rambi
jamaa wa watu waliouawa katika shambulio hilo.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW