1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vifo vilivyotokana na mafuriko Uhispania vyapanda hadi 200

1 Novemba 2024

Waokoaji wamepandisha idadi ya vifo kutokana na mafuruko makubwa zaidi yaliyotokea Uhispania hadi watu 205. Serikali imepeleka askari 500 zaidi kusaidia katika harakati za kuwatafuta manusura.

Mafuriko ya Uhispania
Mafuriko ya Uhispania Picha: Alberto Saiz/AP Photo/picture alliance

Waokoaji wamepandisha idadi ya vifo kutokana na mafuruko makubwa zaidi yaliyotokea Uhispania hadi watu 205. Serikali imepeleka askari 500 zaidi kusaidia katika harakati za kuwatafuta manusura.

Mafuruko hayo ambayo yameharibu magari, kuvunja madaraja na kuifunika miji na tope tangu Jumanne, ndio janga kubwa kabisa la aina hiyo kutokea katika nchi hiyo ya Ulaya katika miongo mingi. Shirika linaloratibu huduma za dharura katika mkoa wa mashariki wa Valencia ulioathiriwa pakubwa limesema watu 202 wamethibitishwa kufa huko.Mafuriko yapelekea watu 95 kufariki dunia Uhispania

Maafisa katika maeneo jirani ya Castilla-La Mancha na Andalusia tayari walikuwa wametangaza vifo vya pamoja vya watu watatu. Waokoaji wakitumia droni na mbwa wa kunusa walipita majini na kwenye vifusi kuwatafuta watu kadhaa ambao maafisa wanaamini bado hawajulikani waliko.

Idara ya hali ya hewa AEMET imeiweka sehemu ya kusini mwa Andalusia katika kiwango cha juu zaidi cha tahadhari ya mvua kubwa zaidi leo. Aidha imeyatahadharisha maeneo ya Valencia na Catalonia.