1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vifo vya genge lenye silaha Haiti vyafikia 109

10 Oktoba 2024

Idadi ya vifo vilivyotokana na mashambulizi ya kikatili ya genge moja lenye silaha nchini Haiti wiki iliyopita imefikia watu 109 huku wengine zaidi ya 40 wakijeruhiwa.

Haiti Port-au-Prince
Maafisa wa polisi wakipiga doria baada ya kuwasambaza waandamanaji mjini Port-au-Prince, Haiti.Picha: Ralph Tedy Erol/REUTERS

Taarifa iliyotolewa jana na mamlaka nchini humo inasema mauaji hayo yalitokea baada ya nyumba na vyombo kadhaa vya usafiri kuchomwa moto kufuatia genge hilo kurusha risasi kwenye mji wa Port Sonde, ulio umbali wa kilomita 100 kutoka mji mkuu, Port-au-Prince.

Soma zaidi: Waziri Mkuu wa Haiti atafuta msaada zaidi dhidi ya magenge

Naibu mkuu wa wilaya ya Saint-Marc, Walter Montas, alitangaza idadi mpya ya vifo hivyo kupitia redio moja hapo jana, likiwa ongezeko la vifo takribani 40 kutoka ile iliyotangazwa awali na Umoja wa Mataifa.

Mauaji hayo yametokea wakati kikosi maalum cha kimataifa kinachoongozwa na askari polisi wa Kenya, kikijaribu kurejesha udhibiti wa serikali ya Haiti, ambako magenge yenye silaha yametwaa maeneo makubwa ya mji mkuu na mikoani, na kumlazimisha waziri mkuu kujiuzulu mapema mwaka huu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW