Vifo vya ripotiwa Bujumbura kufuatia milipuko ya Jumanne
1 Aprili 2026
Huzuni imetanda katika baadhi ya wakaazi wa mitaa mbali mbali ya jiji la Bujumbura. Taarifa zinasema silaha hizo ziloonekana mabaki yake kama mtwangiyo wa kinu zilianguka katika mitaa tafauti ya jiji.
Ikiwa île iliyo karibu na kambi ya Musaga eneo la tukio aidha mitaa ya mbali kama umbali wa kilometa 10 na eneo hilo.
Mtaani Gihosha kaskazini mwa jiji nyumbani kwa sheikh Kida silaha hiyo ilianguka uwani na kumkata mguu binti yake, huku mkewe sheikh na mfanyakazi wake wakijeruhiwa vibaya.
Si mbali na hapo kombora lilianguka nyumbani kwa baba mwengine na kumpiga kichwani na kufariki papo hapo.
"Wako waliokufa na wengine kujeruhiwa"
Gavana wa mkoa wa Bujumbura Aloys Ndayikengurukiye anasema miripuko hiyo kiini chale ni moto uloripuka ndani ya ghala ya silaha katika kambi ya musaga. Na kuwataka raia kusalia watulivu na kurudi katika majukumu yao ya kila siku.
"Baada ya kuwasiliana na maafisa wa jeshi tulitaka kuwatuliza nyoyo raia kwani kumekuwa na taarifa kuwa ni shambulio lilotokea. Tuna wahakikishia kuwa ni moto uloripuka katika ghala ya silama katika kambi ya musaga. Wapo waliokufa na wengine kujeruhiwa kwa sasa tunakusanya matokeo kutoka tarafa mbalimbali", alisema Ndayikengurukiye.
Gavana huyo wa Bujumbura amebaini pia kuwepo na pale makombora hayo yalipoangukia na kusalia bila kuripuka hivyo amewataka raia kutowa taarifa kwa watawala wa jeshi ama kwa walinda usalama, ili kuepusha kusababisha maafa mengine.
Jeshi limejizuwia kutowa taarifa na kwamba matokeo ya hasara ́yatasalia siri jeshini.
Taarifa zinasema shirika la msalaba mwekundu limejielekeza wakati huu ni kiripoti katika jela kuu la mpimba si mbali na eneo la tukio ambako pia makombora hayo yaripotiwa kuangukia na kusabasha pia hasara.