Vigogo wa Kenya waelekea ICC,The Hague
5 Aprili 2011Matangazo
Hatma ya washukiwa sita wanaotuhumiwa kupanga na kufadhili ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 nchini Kenya, waliotajwa na mwendesha mashtaka wa mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, Louis Moreno Ocampo wanaanza safari yao leo kuelekea mjini The Hague, Uholanzi wanakotarajiwa kwenda kujibu mashtaka hayo. Naibu Waziri Mkuu, Uhuru Kenyatta na Mbunge wa Eldoret Kaskazini, William Rutto wanaondoka leo usiku kuelekea The Hague. Hisia mbalimbali zimetolewa na viongozi pamoja na wananchi kuhusiana na kufikishwa mahakamani kwa washukiwa hao.
Mwandishi wetu Alfred Kiti Kutoka Nairobi ametuandalia taarifa hiyo.
Mwandishi: Alfred Kiti
Mpitiaji: Grace Patricia Kabogo
Mhariri:Abdul-Rahman