1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUfaransa

Vijana sita wakutwa na hatia ya mauaji ya mwalimu Ufaransa

9 Desemba 2023

Mahakama ya watoto nchini Ufaransa imewakuta na hatia vijana sita waliohusishwa na mauaji ya mwalimu Samuel Paty, mnamo mwaka 2020.

Mwalimu wa shule ya sekondari Samuel Paty alieuliwa nchini Ufaransa mwaka 2020
Mwalimu wa shule ya sekondari Samuel Paty alieuliwa nchini Ufaransa mwaka 2020Picha: Lp/Olivier Lejeune/dpa/picture alliance

Miongoni mwa washtakiwa hao ni msichana aliyewaambia wazazi wake kwamba mwalimu huyo aliwafukuza darasani wanafunzi wa Kiislamu kabla ya kuwaonyesha wenzao picha ya Mtume Mohammad.

Mahakama imemkuta na hatia msichana huyo kwa kutoa taarifa za uongo, kwa kuwa iliejulikana baadae kwamba hakuwepo darasani wakati huo.

Washtakiwa wengine walikutwa na hatia ya kushiriki katika njama ya uhalifu na kusaidia kuandaa shambulizi.

Paty aliuliwa nje ya shule yake katika kitongoji cha Paris na kijana wa miaka 18 mwenye asili ya Chechnya, ambaye alipigwa risasi na kufa mara baada ya shambulizi hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW