Vijana wa Afrika kupewa kipaumbele asema Macron
11 Oktoba 2018Wanatarajiwa kumchagua mwanasiasa wa Rwanda na kuthibitisha kwa namna hiyo nafasi muhimu inayoshikiliwa na bara la afrika katika jumuia hiyo.
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Rwanda bibi Louise Mushikiwabo, anaungwa mkono na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliyetilia mkazo katika hotuba yake, umuhimu wa kuthamini ujuzi wa lugha tofauti.
"Karibuni katika ardhi ya milele ya Armenia" amesema kwa upande wake waziri mkuu wa Armenia Nikol Pachinian, katika hotuba yake ya ufunguzi aliyoianza kwa kumsifu mwanamuziki wa kifaransa mwenye asili ya Armenia Charles Aznavour aliyefariki dunia hivi karibuni.
Nchi hiyo ndogo ya wakaazi milioni tatu ambao asili mia 6 tu ndio wanaozungumza kifaransa ndio mwenyeji wa tukio hili kubwa la kimataifa; viongozi 26 wa taifa, wawakilishi 3500 wanahudhuria mkutano huu wa 17 wa jumuia ya Francophonie inayaozileta pamoja nchi 84.
Mushikawabo
Mkutano huo wa kilele utamchagua kesho ijumaa-siku ya mwisho ya mkutano huo, mwenyekiti mpya, Louise Mushikiwabo awe katibu mkuu wa jumuia hiyo kwa kipindi cha miaka minne.Waziri huyo wa mambo ya nchi za nje wa Rwanda ana uhakika wa kushinda baada ya Canada,pamoja na Quebec kutangaza wanaacha kumuunga mkono katibu mkuu anaemaliza wadhifa wake Michaelle Jean aliyepaanga kugombea mhula wa pili.
Kuteuliwa kulikothibitika kwa bibi Mushikiwabo ni ushahidi wa kurejea Afrika katika uongozi wa jumuia ya Francophonie ambayo daima ilikuwa ikiongozwa na waafrika kabla ya bibi Jean. Kitovu cha lugha ya kifaransa kinakutikana katika bonde la mto Kongo amesisitiza rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.
"Kipaumbele katika mapambano ya Francophonie kinahusu vijana na hasa wa Afrika amesema rais huyo wa Ufaransa akiungwa mkono na rais Mahamadou Issoufou wa Niger-vijana wanaohitaji kupata elimu ili kukomesha mitindo ya ndowa za kulazimishwa na mimba za kushitukia."
TUnabidi tuwekeze zaidi katika elimu ya vijana amesema kwa upande wake rais wa jamhuri ya safrika kati Faustin-Archange Touadera.
Rais Macrob ameshauri mwongozo wa Francophonie ufanyiwe marekebisho na hasa katika kifungu kinachozungumzia namna ya kujiunga na jumuia hiyo. Suala hilo linazuka katika weakati ambapo Saudi Arabia inaapomba kujiunga na jumuia hiyo kama mwanachama asiyekuwa na haki ya kupiga kura.
Mwandishi:Sekione Kitojo/AFP
Mhariri:Saumu Yusuf