1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vijana wakerwa baada ya machafuko mjini Stuttgart

22 Juni 2020

Mji wa Stuttgart, kusini magharibi mwa Ujerumani umeanza kusafishwa baada ya usiku wa machafuko ambayo hayajawahi kushuhudiwa mjini huko. Wakaazi na baadhi ya vijana wamehoji kilichotokea.

Deutschland Stuttgart Unruhen Vandalismus
Picha: Reuters/R. Brock

"Tulikuwa tukisikiliza muziki, huku wengine wakicheza na kufurahika, mara moja machafuko yakatokea",amesema Julia P. ambaye alirejea kwenye eneo la tukio kushuhudia uharibifu uliofanyika.

Kama vijana wengine, msichana huyo wa miaka 17 alikuwa na marafiki zake kwenye bustani ya katikati mwa mji wa Stuttgart Jumamosi jioni. Amesema aliondoka mapema, lakini punde baadae aliona vidio ya kilichotokea kwenye mtandao wa snapChat.

Kwenye eneo la kibiashara la Konigstrasse, vioo vya maduka vimepasuka na maduka mengine kuvunjwa, ni vigumu kuamini kwamba usiku wa sherehe uligeuke kuwa mmoja wapo ya usiku wa machafuko ambayo hayajawahi kushuhudiwa kwenye mji huo wa Stuttgart.

Answar S., mvulana wa miaka 18 ambae pia alishiriki kwenye tukio hilo amesema kwamba haelewi kwa nini machafuko baina ya polisi na vijana hao, yalisababisha baadhi ya vijana kuharibu maduka.

"Walidhani wako kwenye filamu ya Kimarekani (Hollywood) ambako kila kitu kinaweza kutokea",alisema.

Machafuko yalitokea Jumamosi jioni na Jumapili asubuhi baada ya polisi kuweka vizuwizi kwa ajili ya kuchunguza madawa ya kulevya kwenye eneo muhimu ya mji ya Schlossplatz.

Waziri wa mambo ya ndani ya Ujerumani Horst SeehoferPicha: picture-alliance/dpa/M. Murat

Mashahidi kwenye eneo la tukio wameiambia DW kwamba hali ilizorota wakati polisi ilipomuandama mmoja ya vijana aliejaribu kukwepa uchunguzi wa polisi. Kwa mshikamano vijana wenzake walianza kuwashambulia polisi.

Kanda za vidio zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zimeonyesha vijana wakirusha mawe na vitu vingine kwenye magari ya polisi. Kwenye vidio nyingine mtu alionekana akimsogelea afisa wa polisi aliepiga goti ardhini na kumpiga teke lililo muangusha afisa huyo wa polisi, huku watu wengine wakimfurahia. Maafisa 19 wa polisi walijeruhiwa kwenye machafuko hayo.

Machafuko yalisambaa hadi kwenye eneo la kibiashara, ambako wafanya fujo walivunja maduka. Maduka mengi yaliporwa,ikiwemo duka ya mapambo ya vito, duka la kuuza simu za mkononi na ile ya vifaa vya michezo.

Inakadiriwa kwamba watu 500, wengi wao wakiwa wavulana walihusika katika machafuko hayo. Watu 24 walikamatwa na polisi.

Jummapili jioni, viyoo vilivyopasuka kwenye maduka yaliobomolewa viliogotwa ao kukusanywa.Mabango yalioandikwa "jenga,usibomoe "Wakaazi waliojitokeza jumapili walisimama mbele ya maduka hayo kushuhudia uharibifu uliofanyika.  "Matukio ya aina hii, hayatokee hapa Stuttgart", walikuwa wakielezea wapita njia.

Viongozi wa mji walieleza kwamba machafuo hayo yahakuchochewa kisiasa, ulevi wa pombe ulichangia pakubwa na vilevile shauku kutokana na mitandao ya kijamii.

Polisi wa mjini Stuttgart siku ya JumapiliPicha: picture-alliance/dpa/C. Schmidt

Yusef, kijana wa miaka 19 alieshuhudia machafuko hayo Jumamosi, anasema kuwa sababu kadhaa zilichangia kwenye machafuko hayo, akisema watu wengi walikuwa walevi na kugeuza jioni hiyo kuwa ya machafuko.

"Hasira ilikuwa kubwa na haikudhibitiwa",alisema. Alipoulizwa sababu za hasira hiyo,Yussef alisema vijana wengi waliohusika kwenye machafuko hayo,wakiwemo watu wa rangi, ambao wanahisia kwamba mara nyingi polisi huwalenga.

Uhasama umekuwa mkubwa kutokana pia na maandamano ya hivi karibuni nchini Mrekani kufuatia vitendo vya ukatili vya polisi. Vizuwizi vya kupambana na virusi vya Corona na kero ya janga hilo vilichangia pia kwa aina moja au nyingine, alisema Yussef."Kila kitu kilifungwa" amesema Yussef akielekea kwenye mkoa wa kibiashara ambao hivi sasa maisha yamerudi ya kawaida. Wengi walikerwa na amri ya kutotoka nje,wakiwa na wasiwasi kuhusu ujio wao na wakifurahi kuwa nje pamoja na marafiki zao.

Vingozi wameanzisha uchunguzi mkubwa kuhusu machafuko hayo,kwa kutumia ushahidi walionao kutoka kwenye maduka yalioporwa ilikuwasaka wahusika.

Lakini swali ambalo kila mtu anajiuliza mjini Stuttgart na ambalo si rahisi kupata jibu ni vipi hali hiyo ilifikia hadi kwenye machafuko ya aina hiyo ?

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW