Vijana wakimbia Myanmar kuepuka kujiunga na jeshi
16 Februari 2024Shirika la habari la AFP liliripoti kushuhudia foleni ya kati ya watu 1,000 na 2,000 katika mitaa ya karibu na ubalozi huo ikilinganishwa na idadi ya chini ya watu 100 kabla ya tangazo hilo la siku ya Jumamosi.
Ubalozi huo umesema unatoa tikiti 400 kwa siku ili kushughulikia vyema umati huo.
Hakuna maelezo yoyote yaliyotolewa kuhusu jinsi wale watakaochaguliwa kujiunga na jeshi watakavyohudumu.
Soma zaidi: Myanmar yafanya mgomo baridi katika kumbukumbu ya mapinduzi
Jeshi hilo limesema linaandaa mikakati ya kuwapa silaha wapiganaji wanaoliunga mkono jeshi wakati linapokabiliana na wapinzani kote nchini humo.
Siku ya Jumamosi, msemaji wa jeshi, Zaw Min Tun, alisema mfumo wa huduma za kijeshi unahitajika kwa sababu ya hali inayoendelea nchini humo.