1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vijana 4 wafa kwa kushambuliwa na Viboko Ziwa Naivasha

4 Januari 2026

Vijana wanne wa kiume wamekufa katika shambulio la Kiboko kwenye Ziwa Naivasha nchini Kenya.

Kenya | Ziwa Naivasha
Kenya | Ziwa NaivashaPicha: DW/B. Maranga

Vijana wanne wa kiume wamekufa katika shambulio la Kiboko kwenye Ziwa Naivasha nchini Kenya. Vijana wapatao 14 walishambuliwa wakati wakijaribu kuvua samaki usiku wa Ijumaa katika ufuo wa Ziwa Naivasha.

Eneo hilo ni kivutio maarufu cha utalii kilichoko kilometa 80 kutoka mji mkuu wa Nairobi katika bonde la Ufa. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Kenya, viboko kadhaa waliwashambulia vijana hao huku baadhi wakifanikiwa kuogelea na kufika eneo salama lakini wengine walishambuliwa au kuzama.

Kulingana na jamaa zao, vijana hao walikuwa wakitafuta kuongeza kipato cha familia zao kupitia uvuvi. Viboko, ambao hula majani kwenye ufuo wa ziwa wakati wa usiku, wanaweza kuwa wakali pale wanapohisi eneo lao limevamiwa. Waendeshaji wa hoteli za kitalii na kambi huwaonya wageni dhidi ya kutembea usiku kando ya ziwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW