1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vijana washauriana umuhimu wa kupima virusi vya HIV

Veronica Natalis
1 Desemba 2025

Ulimwengu unaadhimisha siku ya kupambana na Ukimwi. Pamoja na mambo mengine, siku hii ni mahususi kwaajili ya kutathimini harakati za kutokomoza maambukizi mapya na vifo vitokanavyo na ukimwi.

Siku ya Ukimwi Duniani
Moja kati ya njia inayotumiwa kufikia malengo hayo ni elimu ya upimaji na matumizi sahihi ya dawa za kupunguza makali ya virusi vya HIV.Picha: picture-alliance/AP Photo/A. Carconi

Kundi la  vijana wapatao 20 kutoka kituo cha vijana wanaoishi na maambukizi vya virusi vya HIV mjini Arusha Tanzania, walio chini ya umri wa miaka 25, wengi wao walitambua kwamba wanaishi na maambukizi hayo,  tangu wakiwa na umri mdogo. 

Waliambukizwa kutoka kwa wazazi wao wakati wa kuzaliwa, njia hiyo ikijulikana kitaalamu kama maambukizi ya mama kwenda kwa mtoto.

Wengi wao ni wanafunzi wa sekonadari na vyuo, walitambua hali zao baada ya kupima na wakaamua kujiunga katika kundi hili ili waweze kupata elimu ya mafunzo ya kujikinga na maambukizi mapya kiurahisi lakini kupata elimu ya kuwasaidia kutimiza ndoto zao.

Vituo vya haraka vya kupima virusi vya HIV vinavyosababisha ugonjwa wa UkimwiPicha: Getty Images/AFP/Y. Chiba

Vijana hawa wamekubali jamii itambue kwamba wanaishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi, na wanaeleza kwamba wamechagua njia hiyo ili iwe rahisi kuwasaidia vijana wengine ambao hawatambui hali zao za kiafya, kujikinga na maambukizi, ama wanaotambua hali zao lakini wakakata tamaa ya kutimiza ndoto zao.

Juhudi zao zimefanikiwa kwa kiasi gani?

Kupitia juhudi hizo vijana hawa wameweza kuwafikia vijana wengine ambao wanafanya biashara ya ngono, wanaotumia dawa za kulevya na mazingira mengine hatarishi kuwapa elimu na kuwahamasisha kupima afya zao. 

Kulingana na wataalamu wa afya, maambukizi ya virusi vya HIV yanaweza kupitishwa kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto yanaweza kupitishwa wakati mtoto akiwa tumboni, wakati wa kujifungua na wakati wa kunyonyesha.

Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zimeweka mikakati ya kupunguza maambukizi hayo huku miongoni ikiwa ni upimaji wa mama wajawazito pamoja na matibabu ya dawa za kupunguza makali ya virusi vya HIV kwa mama wajawazito walio na maambukizi hayo.

Je hofu ya ukimwi kwa vijana imepungua?

02:59

This browser does not support the video element.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW