1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Vikao vya kusikiliza kesi za kumzuia Trump asigombee vyaanza

30 Oktoba 2023

Kampeni ya kujaribu kumzuia rais wa zamani Donald Trump kugombea urais kwa mara nyengine, inaingia awamu mpya wiki hii.

Donald Trump, rais wa zamani wa Marekani.
Donald Trump, rais wa zamani wa Marekani.Picha: ALEX KENT/AFP/Getty Images

Vikao vya kusikiliza kesi ambazo huenda zikaishia Mahakama ya Juu vitaanza katika majimbo mawili.

Kampeni hiyo inaegemea ibara ya katiba ya Marekani inayowazuia waliotiwa hatiani kwa makosa ya uasi na kutumia nguvu dhidi ya taasisi za dola, kutogombea Urais.

Wanaoendesha kampeini za kutaka Trump asiwanie Urais wanajenga hoja kwamba alikiuka ibara hiyo ya katika kwa kuchochea uvamizi wa majengo ya bunge Januari 6 mwaka 2021.

Kikao cha kusikiliza kesi ya kumzuia Trump kutoshiriki uchaguzi kinaanza jimboni Colorado Jumatatu huku kukitarajiwa majibizano katika Mahakama ya Juu ya Minnesota siku ya Alhamis, katika juhudi za kuzuia mgombea huyo wa chama cha Republican kutogombea katika jimbo hilo.

Iwapo majaji katika kesi hizo wataamua kumzuia Trump ashiriki kura au la, ni maamuzi yatakayokatiwa rufaa kwa haraka katika Mahakama ya Juu.