VIKOSI KULINDA AMANI BURUNDI:
23 Desemba 2003Matangazo
NEW YORK: Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan sasa anaweza kutayarisha mipango ya kupeleka tume ya kulinda amani nchini Burundi.Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika hati yake limetoa muito kwa Kofi Annan kuanza kukadiria vipi Umoja wa Mataifa utaweza kusaidia kuyatekeleza makubaliano ya amani yaliopatikana mapema mwaka huu.Kikosi cha amani cha askari 2,600 kutoka nchi za Kiafrika kilipelekwa Burundi mwezi Machi kuhakikisha kuwa mapigano yamesitishwa.Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu miaka kumi nchini Burundi vimepoteza maisha ya watu 300,000.