1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikosi vya Israel vyauwa Wapalestina 7 Ukingo wa Magharibi

Hawa Bihoga
19 Oktoba 2023

Vikosi vya Israel vimewauwa Wapelestina saba katika matukio tofauti kwenye Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu, huku idadi ya vifo ikizidi kuongezeka katika maeneo hayo na vita vikizidi kurindima Gaza.

Gazastreifen | Tite und Verletzte nach Luftangriff in Rafah
Wapalestina wakiwanasuwa jamaa zao kutoka vifusi vya majengo yaliyoteketezwa na mashambulizi ya Israel katika mtaa wa Rafah mjini Gaza.Picha: MOHAMMED ABED/AFP

Wizara ya afya ya Palestina imesema Wapalestina wasiopugua 73 wameuawa na vikosi vya Israel au na walowezi wa Kiyahudi katika Ukingo wa Magharibi tangu kuzuka kwa mzozo wa Gaza Oktoba 7.

Jeshi la Israel halijazugumzia matukio hayo, lakini taarifa yake imesema wanajeshi wanaendelea na operesheni ya kuzuwia matukio ya kigaidi. 

Soma zaidi: Israel na Misri zaruhusu misaada ya kibinaadamu kupelekwa Gaza

Israel imelikalia kimabavu eneo la Ukingo wa Magharibi tangu vita vya mwaka 1967 kati yake na mataifa ya Kiarabu, na vikosi vyake hufanya uvamizi wa mara kwa mara dhidi ya jamii za Kipalestina.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW