1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Syria yajipanga kulipiza mashambilio ya waasi mkoani Hama

3 Desemba 2024

Vikosi vya kijeshi vya Syria vinaendelea kuimarisha nguvu zao kulinda maeneo ya mkoa wa Hama ili kuanza kujibu mashambulizi ya makundi ya waasi wenye silaha. Hayo yameripotiwa na kituo cha habai cha serikali ya Syria.

Syria
Vikosi vya jeshi la Syria vyajipanga kulipiza mashambilio ya waasi katika maeneo ya mkoa wa HamaPicha: LOUAI BESHARA/AFP

Wakati huohuo Qatar kupitia msemaji wa wizara yake ya mambo ya kigeni imesema inashirikiana na Uturuki pamoja na washirika wengine wa kikanda kutafuta suluhisho la kumaliza mapigano Syria. 

Vikosi vya Syria vyashambulia vijiji kaskazini mwa Syria na kuongeza wasiwasi kwa jirani yake, Iraq

Kuafuatia mapigano yaliyoibuka nchini Syria, Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk ameelezea wasiwasi wake kuhusu kuongezeka kwa vita Kaskazini magharibi mwa Syria.

Ameyasema hayo huku ofisi yake ikitafuta taarifa kuthibitisha idadi ya mashambulio ya umwagaji damu yaliyofanywa na pande zote mbili, vikosi vya jeshi la serikali na waasi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW