1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Vikosi vya Marekani vyaondoka katika kambi yao Niamey, Niger

8 Julai 2024

Wanajeshi wa Marekani wamekamilisha mchakato wa kuondoka katika kambi yao kwenye mji mkuu wa Niger, Niamey na wataondoka kikamilifu kutoka eneo la Agadez kaskazini mwa nchi hiyo kabla ya tarehe ya mwisho ya Septemba 15

Niger Niamey 2024 | US-Militär beginnt offiziellen Rückzug
Picha: ISSIFOU DJIBO/EPA

Katika taarifa, nchi hizo mbili zimesema kuwa wizara ya ulinzi ya Niger na Idara ya Ulinzi ya Marekani zimetangaza kukamilika kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani na vifaa kutoka kambi 101 huko Niamey.

Soma pia:Ujumbe wa Marekani wajadili kuondoka kwa wanajeshi Niger

Ndege ya mwisho iliyobeba wanajeshi wa Marekani ilitarajiwa kuondoka Niamey jana jioni.

Ujerumani kumaliza operesheni zake Niger

Siku ya Jumamosi, wizara ya ulinzi ya Ujerumani pia ilisema itakamilisha operesheni zake katika kambi yake nchini Niger kufikia Agosti 31 kufuatia kuvunjika kwa mazungumzo na viongozi wa kijeshi.