1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikosi vya Pakistan vyawasaka wafuasi wa Imran Khan

Josephat Charo
27 Novemba 2024

Uvamizi mkubwa umefanywa na maafisa wa usalama katikati mwa mji mkuu Islamabad huku kukiwa na giza baada ya taa kuzimwa na mabomu ya kutoa machozi kufyetuliwa.

Polisi wakifyetua gesi ya machozi kuwatawanya waandamanaji Islamabad
Polisi wakifyetua gesi ya machozi kuwatawanya waandamanaji IslamabadPicha: Irtisham Ahmed/picture alliance/AP

Vikosi vya usalama vya Pakistan vimeanzisha msako wa usiku dhidi ya wafuasi wa waziri mkuu wa zamani anayetumikia kifungo jela tangu Agosti mwaka uliopita, Imran Khan, ambao waliandamana na kufanikiwa kufika katikati ya mji mkuu Islamabad kudai aachiwe huru hapo jana Jumanne.

Vyombo vya habari vimeripoti kwamba mamia ya waandamanaji wametiwa mbaroni. Awali maalfu ya waandamanaji walikuwa wamekusanyika katikati ya mji wa Islamabad baada ya msafara ulioongozwa na mke wa Khan, kuvuka vizuizi kadhaa vya usalama hadi kufikia eneo lenye ulinzi mkali.

Eneo hilo linalolindwa na wanajeshi ndiko kunakopatikana afisi muhimu na majengo, likiwemo bunge na balozi kadhaa za nchi za kigeni.

Watu wapatao sita, wakiwemo wanajeshi wanne, waliuwawa kabla msako wa jana Jumanne kuanzishwa.

Chama cha Khan cha Pakistan Tehreek-e-Insaf (PTI) kimesema kinapanga kufanya mgomo katika eneo hilo hadi Khan aachiwe huru.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW