1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSyria

Vikosi vya Syria vyaendelea kukabiliana na waasi Aleppo

2 Desemba 2024

Jeshi la anga la Syria kwa ushirikiano na vikosi vya Urusi walishambulia maeneo yanayodhibitiwa na waasi mashariki mwa mji wa Aleppo na kusababisha vifo na majeruhi miongoni mwa waasi hao.

Syria Aleppo 2024 | Waasi wapambana dhidi ya vikosi vya taifa
Vikosi vya serikali ya Syria vyakabili mashambulizi makubwa kuwahi kutokea nchini humo katika miaka ya hivi karibuni.Picha: Abdulfettah Huseyin/Anadolu/picture alliance

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na ofisi ya Waziri Mkuu wa Syria.

Syria imewapeleka kwa haraka wanajeshi wa ziada kaskazini magharibi mwa nchi hiyo katika juhudi za kuwarejesha nyuma waasi hao waliofanya mashambulizi ya kushtukiza na ambao sasa wanadhibiti mji wa Aleppo.

Marekani, Ujerumani, Ufaransa na Uingereza wametoa wito wa usitishwaji wa mapigano nchini Syria wakitaka kulindwa kwa raia na miundo mbinu, huku Iran na Urusi zikisema zitaendelea kumuunga mkono rais wa Syria Bashar al-Assad na kumsaidia kukabiliana na waasi hao.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu ilisema zaidi ya watu 14,000 - karibu nusu wakiwa watoto - wamekimbia makazi yao kutokana na ghasia hizo.  

Mashambulizi hayo yamezuka wakati nyeti kwa Syria na eneo hilo la Mashariki ya Kati. Ikiwa ni siku mbili tu baada ya hatua tete ya usitishaji wa mapigano kati ya kundi la Hezbollah na Israel katika nchi jirani ya Lebanon.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW