1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Wanajeshi wa Ufaransa wameanza kuondoka nchini Niger

11 Oktoba 2023

Ufaransa imeanza kuondoa wanajeshi wake kutoka Niger baada ya kuamriwa kufanya hivyo na utawala wa kijeshi nchini humo

Wanajeshi wa Ufaransa washika doria katika eneo la Madama karibu na mpaka na Libya mnamo Januari 1 2015
Wanajeshi wa Ufaransa washika doria katika eneo la Madama karibu na mpaka na LibyaPicha: Dominique Faget/AFP

Msemaji wa mkuu wa jeshi la Ufaransa, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba kundi la kwanza tayari limeondoka nchini humo, hatua inayothibitisha tangazo la siku ya Jumatatu la utawala huo wa kijeshi wa Niger kwamba kikosi cha wanajeshi 1400 wa Ufaransa wataanza kuondoka nchini humo kuanzia siku ya Jumanne.

Soma pia:Nigeria yapongeza pendekezo la Algeria kuwa mpatanishi Niger

AFP imeripoti kuwa msafara wa wanajeshi pamoja na malori ya kusafirisha vifaa na magari ya vita kutoka Magharibi mwa Niger uliwasili katika mji mkuu wa Niamey mwendo wa saa sita mchana hapo jana.

Marekani yakatiza msaada kwa Niger

Haya yanajiri wakati Marekani ikikatiza jana msaada wa zaidi ya dola milioni 500 kwa taifa hilo la Niger. Marekani ilitangaza kuwa jeshi la Niger lilifanya mapinduzi mnamo Julai 26, na kuidondoa madarakani serikali ya kidemokrasia.

Soma pia: Blinken azungumza na Bazoum kwa njia ya simu

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani Matthew Miller, amesema kurudishwa kwa msaada wa nchi yake kwa Niger, kutahitaji kuchukuliwa kwa hatua za kurejesha uongozi wa kidemokrasia katika muda wa haraka.

 

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW