Vikosi vya Uganda vyaingia katika mji wa Bunagana, Kongo
31 Machi 2023Haya ni kwa mujibu wa kamanda wa kikosi hicho cha Afrika Mashariki, Jenerali Jeff Nyagah wa Kenya.
Soma pia:Maoni mseto yatolewa baada ya Uganda kupeleka wanajeshi wake katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Nyagah amewaambia waandishi wa habari kwamba, wanajeshi elfu moja wa Uganda wamevuka mpaka na kuingia kwenye mji huo unaopakana na Uganda ambapo sasa idadi jumla ya kikosi cha wanajeshi itakuwa elfu mbili.
Mkaazi mmoja wa Bunagana pia amelithibitishia shirika la habari la Ufaransa AFP kuingia kwa vikosi hivyo. Jana jioni, Rais wa Uganda Yoweri Museveni, alisema kwamba wanajeshi hao hawatopambana na waasi wa M23.
Soma pia: Uganda yajiandaa kupeleka wanajeshi 1,000 mashariki mwa Kongo
Wanajeshi hao wanatarajiwa kusimamia kuondoka taratibu kwa waasi wa M23 ambao wameyateka maeneo kadhaa mashariki mwa Kongo tangu kuanza mapambano mwishoni mwa mwaka 2021.