1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikosi vya Ukraine vinasonga mbele Bakhmut

14 Agosti 2023

Vikosi vya Ukraine vinapiga hatua katika juhudi za kulikombowa eneo lililoko karibu na mji unaodhibitiwa na Urusi wa Bakhmut mashariki mwa Ukraine.

Ukraine Krieg | Ukrainische Soldaten an der Front bei Bachmut
Picha: 3rd Assault Brigade/ Ukrainian Armed Forces Press Service/REUTERS

Kwa ujumla vikosi vya wanajeshi wa Ukraine kuzunguka mji huo wa Bakhmut vimekomboa eneo la kilomita 40 za mraba tangu vilipoanza operesheni yao ya kujibu mapambano zaidi ya wiki 10 zilizopita kwa mujibu wa naibu waziri wa ulinzi wa nchi hiyo Hanna Malia. Taarifa pia zimeeleza kwamba kuna mapigano makali katika majimbo ya  Kharkiv na Luhansk na karibu na Kupyansk na Lyman. Aidha naibu waziri huyo wa ulinzi wa Ukraine amethibitisha kwamba wanajeshi wa nchi hiyo pia wameshasogelea eneo la karibu na mto Dnipro katika jimbo la Kherson linalodhibitiwa na Urusi.Mapambano hayo yanaripotiwa katika wakati ambapo waziri wa fedha wa Ujerumani  Christian Lindner yuko ziarani mjini Kiev alikowasili leo kwaajili ya mazungumzo ya kisiasa na maafisa wa ngazi za juu wa Ukraine.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW