1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Vikosi vya Ukraine vyakabiliana na askari 50,000 wa Urusi

11 Novemba 2024

Vikosi vya Ukraine vimo katika makabiliano makali na wanajeshi wapatao elfu 50,000 wa Urusi katika mkoa wa Kursk. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumatatu na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.

Vita vya Ukraine - Kursk
Mkoa wa Kursk nchini Urusi umeshuhudia mashambulizi makali kati ya vikosi vya Ukraine na UrusiPicha: Rusian Defense Ministry Press Service/AP/dpa/picture alliance

Rais Zelensky ameongeza kuwa Ukraine itaimarisha vikali safu yake kwenye maeneo ya Pokrovsk na Kurakhove mashariki, ambako mapigano yamepamba moto.

Soma pia: Urusi na Ukraine zashambuliana vikali na droni baada ya mazungumzo ya simu ya Trump na Putin

Kwingineko, watu wasipungua 7 wamejeruhiwa katika shambulizi la kombora la Urusi katika mji wa Kryvyi Rih kusini mashariki mwa Ukraine. Mji huo ndiko anakotokea Rais Zelensky.

Kiongozi huyo amesema Urusi inatafuta kuendeleza vita na kila shambulio linaashiria kuwa Moscow haiko tayari kwa suluhisho la kidiplomasia. Zelensky amerejelea wito wake wa kupatiwa silaha zaidi ili kuitetea nchi yake dhidi ya mashambulizi ya Urusi.