1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikosi vya Ukraine vyasonga mbele Bakhmut

Josephat Charo
29 Juni 2023

Vikosi vya Ukraine vinasonga mbele pole pole lakini kwa uhakika katika uwanja wa vita mashariki na kusini mashariki mwa nchi pamoja na eneo la Bakhmut.

Kämpfe und Zerstörung in Bachmut, Ukraine
Picha: LIBKOS /AP/picture alliance

Jenerali mkuu wa jeshi la Ukraine Valery Zaluzhniy amemfahamisha mwenyekiti wa kamati ya pamoja ya wanadhimu wa jeshi Marekani Mark Milley kwamba vikosi vyake vimefanikiwa kuyakomboa maeneo ya Bakhmut yaliyotekwa na vikosi vya Urusi mwezi uliopita katika mapambano makali.

Zaluzhniy amemfahamisha Milley kuhusu silaha zinazohitajika na vikosi vya Ukraine pamoja na vifaa vya kuyategua mabomu ya kutegwa ardhini.

Wakati haya yakiarifiwa maafisa wa Ukraine wamesema idadi ya vifo kutokana na shambulizi lililofanywa na vikosi vya Urusi kwenye mgahawa katika mji wa mashariki wa Kramatorsk siku mbili zilizopita imefikia 12.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW