SiasaDenmark
Vikosi kutoka nchi za Ulaya vyaendelea kuwasili Greenland
16 Januari 2026
Matangazo
Hii ni baada ya mazungumzo kati ya Marekani na wawakilishi wa Denmark na Greenland kushindwa kufikia muafaka kuhusu mustakabali wa kisiwa hicho cha Aktiki.
Ikulu ya White House imesisitiza kuwa kitakachofuata kwa sasa ni "mazungumzo ya kiufundi" kuhusu makubaliano yatakayoiwezesha Marekani kuinunua Greenland.
Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Denmark Lars Løkke Rasmussen amekanusha kauli hiyo na kusema kumeundwa timu itakayojadili namna ya kutatua tofauti zilizopo kati ya mataifa hayo.