1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Vikosi vya Urusi vimelikamata eneo la makaazi Donetsk

9 Julai 2024

Wizara ya ulinzi ya Urusi imefahamisha kwamba,vikosi vya nchi hiyo vimedhibiti eneo la makaazi la Yasnobrodivka, katika mkoa wa Donetsk huko mashariki mwa Ukraine.

Ukraine | Donetsk
Nyumba iliyoharibiwa mkoani DonetskPicha: Jose Colon/Anadolu/picture alliance

Wizara ya ulinzi ya Urusi imefahamisha kwamba,vikosi vya nchi hiyo vimedhibiti eneo la makaazi la Yasnobrodivka, katika mkoa wa Donetsk huko mashariki mwa Ukraine. Taarifa hizo zimeripotiwa na shirika la habari la TASS. Shirika la habari la Reuters lililochapisha taarifa hiyo limesema halikuweza kuthibitisha kuhusu tukio hilo.

Soma: Ukraine yasema kijiji kimoja kimekombolewa upande wa kusini

Ripoti pia zinasema katika mji mkuu wa Ukraine, Kiev, shughuli za uokoaji katika hospitali ya watoto iliyoshambuliwa kwa kombora na Urusi, zinaendelea kwa siku ya pili,huku idadi ya waliouwawa ikitajwa kufikia watu 42.

Takriban watu 200 wengine walijeruhiwa katika mashambulizi yaliyofanywa dhidi ya miji kadhaa ya Ukraine.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW