1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Vikosi vya Urusi vyadai kupata mafanikio Ukraine

30 Januari 2023

Vikosi vya Urusi vimedai kupata mafanikio kwenye uwanja wa vita huko mashariki mwa Ukraine baada ya mapambano makali ambayo serikali mjini Kyiv imeyataja kuwa hujuma zisizojali maisha ya watu.

Ukraine Soledar Wagner Söldner
Picha: ITAR-TASS/IMAGO

Mkuu wa maeneo yanayodhibitiwa na Urusi katika mkoa wa Donetsk, Denis Pushilin, amesema vikosi vya Moscow vimesonga mbele na kudhibiti sehemu ya mji wa Vuhledar ambao umekua ngome ya wapiganaji wa Ukraine kwa wiki kadhaa.

Taarifa hizo zinafuatia mashambulizi makali yaliyofanywa na Urusi dhidi ya miji ya mashariki ya Kharkiv, Bakhmut na Avdiivka katika kipindi cha saa 24 zilizopita.

soma zaidi:Zelensky: 2023 utakuwa mwaka wa ushindi kwa Ukraine

Rais Volodymyr Zelenskiy amesema Ukraine inapitia kipindi kigumu huko Donetsk na inahitaji msaada wa haraka wa silaha na aina mpya ya zana za kivita.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW