1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikosi vya Urusi vyadai kusonga mbele mashariki mwa Ukraine

Sylvia Mwehozi
27 Oktoba 2024

Urusi imesema vikosi vyake vimezidi kusonga mbele zaidi mashariki mwa Ukraine na kukidhibiti kijiji kimoja kilichoko uwanja wa mapambano, kilometa chache kutoka mji muhimu wa kiviwanda wa Ukraine ambao unadhibitiwa.

Mashambulizi ya Urusi huko Ukraine
Mashambulizi ya Urusi huko UkrainePicha: State Emergency Service of Ukraine in Dnipropetrovsk region/Handout/REUTERS

Urusi imesema vikosi vyake vimezidi kusonga mbele zaidi mashariki mwa Ukraine na kukidhibiti kijiji kimoja kilichoko uwanja wa mapambano, kilometa chache kutoka katika mji muhimu wa kiviwanda wa Ukraine ambao unadhibitiwa.

Katika taarifa yake ya kila siku, wizara ya ulinzi ya Urusi imeripoti kukikomboa kijiji cha Izmailovka ambacho kabla ya mzozo huo kilikuwa na idadi ya watu chini ya 200. Kwa miezi kadhaa Moscow imepata mafanikio makubwa kwenye uwanja wa vita, ikivishinda vikosi vya Ukraine vilivyolemewa na vichache.

Tangazo hilo limetolewa saa chache baada ya Urusi kudai kuzidungua drone zipatazo 51 za Ukraine zilizoelekezwa katika mikoa yake tofauti ikiwemo karibu na mpaka. Rais wa Urusi Vladimir Putin ameonya leo kwamba Moscow, itajibu vikali endapo nchi za Magharibi zitairuhusu Ukraine kutumia makombora ya masafa marefu dhidi ya ardhi yake.