Vikosi vya Urusi vyaendeleza mashambulizi Ukraine
6 Februari 2023Ofisi ya rais wa Ukraine imesema leo kuwa mapigano makali yanaendelea katika mji wa Bakhmut na miji midogo iliyoko karibu ya Soledar na Vuhledar.
Gavana Serhii Haidai wa mkoa wa Luhansk amesema mashambulizi yamepungua kwa sababu vikosi vya Urusi vimekuwa vikibana matumizi ya risasi kwa ajili ya mashambulizi makubwa zaidi.
Wachambuzi wa kijeshi wanasema vikosi vya Kremlin huenda vinachunguza ngome za Ukraine kubaini maeneo ya udhaifu au vinajaribu kuwavuruga wakati vikijiandaa kwa mashambulizi makubwa kusini mwa Ukraine.
Rais wa Urusi Vladmir Putin anapambana kupata ushindi katika uwanja wa kivita, hasa kuyadhibiti kikamilifu maeneo aliyoyanyakuwa kinyume cha sheria mashariki mwa Ukraine, kabla kuadhimisha mwaka mmoja wa uvamizi wake hapo Februari 24.