1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Vikosi vya Urusi vyaendeleza mashambulizi ya droni Kharkiv

3 Aprili 2026

Picha za video za Reuters Television zilionyesha wazima moto wakimimina maji kwenye nyumba iliyokuwa bado inatoa moshi baada ya kushambuliwa na droni.

Ukraine, Kharkiv 2026 | Wokoaji wazima moto wakizima moto baada ya shambulizi la droni la Urusi katika eneo la makazi
Urusi inaendeleza mbinyo dhidi ya Ukraine, katika wakati ambapo nadhari ya ulimwengu iko kwenye vita vya IranPicha: Andrii Marienko/AP Photo/picture alliance

Mashambulizi ya droni ya Urusi yameendelea kuulenga mji wa Kharkiv kwa siku nzima, huku watu wasiopungua wawili wakijeruhiwa, akiwemo mtoto wa miaka nane.

Meya wa jiji hilo, Ihor Terekhov, amesema mashambulizi yalilenga maeneo manne tofauti, huku zaidi ya droni 20 zikiripotiwa kulipuka ndani ya jiji na kusababisha moto katika baadhi ya majengo.

Picha za Reuters zimeonyesha wazima moto wakizima moto kwenye nyumba iliyoharibiwa vibaya baada ya kushambuliwa, huku samani na sehemu za ndani zikiharibika.

Milipuko mingine iliripotiwa usiku wa manane, hali inayoonyesha mashambulizi hayo kuendelea bila kukoma.

Katika mji wa , shambulizi jingine la Urusi liliharibu jengo la makazi na biashara, ingawa hakuna majeruhi waliothibitishwa.

Wakati huo huo, ndani ya Urusi katika eneo la Belgorod Region, watu 13 wamejeruhiwa kufuatia mashambulizi ya droni kutoka Ukraine, huku mifumo ya ulinzi wa anga ikidungua droni nyingine karibu na Moscow.

Ukraine yarusha makombora ya ATACMS kuelekea Urusi

02:30

This browser does not support the video element.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW