1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Urusi yaongeza mashambulizi mashariki mwa Ukraine

12 Novemba 2023

Vikosi vya Urusi vimeongeza mashambulizi mashariki mwa Ukraine, katika juhudi za kujiimarisha karibu na miji miwili muhimu.

Roketi ikirushwa na vikosi vya Ukraine kutoka Bakhmut
Roketi ikirushwa na vikosi vya Ukraine kutoka BakhmutPicha: SERHII NUZHNENKO/RL/RFE/REUTERS

Maafisa wa jeshi wa Ukraine wamesema vikosi vya Urusi vimeanza mapambano makali karibu na mji wa Bakhmut,kujaribu kutwaa tena udhibiti wa mji huo uliowahi kuwa eneo la umwagaji damu katika vita vinavyoendelea,kabla ya kuangukia mikononi mwa vikosi hivyo mwezi Mei.

Soma zaidi: Waukraine takriban milioni 5 wageuka wakimbizi wa ndani nchini mwao

Wanajeshi wa Ukraine waliukomboa mji huo baadae na kusogea  hadi magharibi mwa Bakhmut, kaskazini na Kusini baada ya serikali ya nchi hiyo kuanzisha operesheni yake kubwa ya msimu wa joto, kujibu mashambulizi ya Urusi. 

Afisa wa jeshi la Ukraine kanali jenerali  Oleksandr Syrskyi amesema  Kuelekea mji wa Bakhmut wanajeshi wa Urusi wameongeza mashambulizi na wanajaribu kuyateka tena maeneo waliyoyapoteza,ingawa wanajeshi wa Ukraine wanapambana kurudisha mashambulizi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW