Vikosi vya Urusi vyashambulia Odesa kwa droni
22 Aprili 2025
Vikosi vya Urusi vimefanya shambulizi kubwa la droni usiku kucha katika maeneo ya makazi ya mji wa bandari wa Bahari Nyeusi wa Odesanchini Ukraine.
Maafisa katika mji huo wamesema mapema leo kwamba shambulizi hilo limesababisha moto na kuharibu makazi mengi.
Meya wa mji wa Odesa Hennadiy Trukhanov ameandika katika mtandao wa Telegram kwamba adui ameyalenga maeneo ya makazi katika eneo linalokaliwa na idadi kubwa ya watu katika wilaya ya Odesa.
Gavana Oleh Kiper amesema shambulizi hilo limeharibu makazi, miundombinu ya umma, taasisi ya elimu na magari.
Wakati hayo yakiarifiwa, Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema serikali yake italifanyia tathmini na kulichambua pendekezo la Ukraine la kusitisha mashambulizi ya kutokea angani katika maeneo ya makazi ya watu.