1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Vikosi vya Urusi vyashambulia vikali mji wa Bakhmut, Ukraine

13 Februari 2023

Mashambulizi makali ya makombora ya vikosi vya Urusi, yameripotiwa leo katika mji wa Bakhmut ulioko mashariki mwa Ukraine.

Russland - Ukraine - Konflikt - Bakhmut
Picha: Yasuyoshi Chiba/AFP

Maafisa wa jeshi la Ukraine wamesema hayo leo mnamo wakati vikosi vya Ukraine vikitarajia mashambulizi zaidi ya ardhini ya  vikosi vya Urusi.

Naibu kamanda wa kikosi kimoja amesema ulinzi mkali umeimarishwa katika maeneo ya  Bakhmut  na watu wenye majukumu ya kijeshi pekee ndio wanaoruhusiwa, kwa hivyo raia wanataka kuondoka, wanaweza kushambuliwa.

Kwa miezi kadhaa, vikosi vya Urusi vimekuwa vikifanya mashambulizi makali kwa lengo la kuukamata Bakhmut na jimbo zima la Donetsk, hali ambayo imesababisha uharibifu mkubwa.

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema leo kwamba vikosi vyake vimekamata Kijiji cha Krasna Gora na kingine kilichoko mkabala cha Paraskoviivka.