1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikosi vya usalama nchini Syria vimewauwa waandamanaji 25

20 Agosti 2011

Watu 25 wameuwawa na vikosi vya Syria baada ya maelfu kumiminika mitaani baada ya sala ya ijumaa. Mauaji hayo yametokea siku moja tu baada ya viongozi wa mataifa makubwa kutoa wito kwa Rais Bashar al-Assad kujiuzulu.

Waandamanaji wa SyriaPicha: picture-alliance/dpa

Mikusanyiko ya ijumaa imekuwa mtihani kwa Assad aliemuhakikishia Katibu Mkuu wa Umoja Ban Ki-moon kwamba vikosi vyake vimemalizia operesheni dhidi ya raia.

Kwa mujibu wa ripoti iliyowasilishwa katika Baraza la Usalama la umoja huo alhamisi iliyopita, sasa idadi ya watu waliouwa katika operesheni za vikosi vya usalama imepindukia 2,000.

Mkuu wa Shirika la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, Navi Pillay ameliambia Baraza la Usalama kwamba " kuna ushahidi wenye uthibitisho" kwamba vikosi vya usalama vya Syria makusudi, vinawavyatulia risasi waandamanaji wanaopinga utawala wa nchi hiyo.

Mwandishi Sudi Mnette
Mhariri: Prema Martin

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi

Gundua zaidi

Onesha taarifa zaidi