Magenge ya uhalifu yajaribu kuvamia Benki Kuu Haiti
20 Machi 2024Benki Kuu ya Jamhuri ya Haiti BRH ni moja ya taasissi chache muhimu ambazo zilikuwa zikiendesha shughuli zake katika mji mkuu huo, ambao umezunguukwa na makundi yanayomiliki silaha kwa takriban wiki tatu sasa.
Kumeshuhudiwa majaribio kadhaa ya kuvamia bank hiyo, lakini hayakufua dafu kutokana na walinzi wa benk na polisi kuzima mashambulizi hayo.
Haiti imekumbwa na ongezeko la ghasia za magenge tangu mwishoni mwa mwezi Februari wakati makundi yenye silaha yalipovamia gereza, na kuwaachia maelfu ya wafungwa.
Soma pia:Magenge ya wahalifu nchini Haiti yaendeleza mashambulizi kwenye makazi ya watu
Wiki iliyopita Waziri Mkuu Ariel Henry alikubali kujiweka kando ili kuruhusu kuundwa kwa serikali ya mpito, kufuatia shinikizo kutoka kwa nchi jirani za Karibian na Marekani.
Viongozi wa Karibiani wamesema makundi yote na vyama vya kisiasa isipokuwa kimoja vimewasilisha wagombeaji wa baraza la mpito la rais watakaokuwa na jukumu la kuchagua waziri mkuu wa mpito Haiti.
Kwa habari nyingine zaidi, karibu kwenye chaneli yetu ya YouTube hapa