1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMyanmar

Vikwazo dhidi ya Myanmar chagizo kwa demokrasia

Hawa Bihoga
4 Septemba 2023

Malaysia imetoa wito leo kwa washirika wake wa Kusini-mashariki mwa Asia, dhidi ya Majenerali wanaotawala Myanmar ikiwa ni pamoja na "vikwazo" vilivyowekwa vimezuia mpango wa amani kwa nchi hiyo iliyokumbwa na mapigano.

Indonesia ASEAN
Mawaziri na maafisa wa ngazi za juu ASEA wakiwa katika mkutano wa 27Picha: Mast Irham/AP Photo/picture alliance

Ujumbe huo usio wa kawaida kutoka kwa Malaysia umetolewa wakati wanadiplomasia wakuu wa Kusini-mashariki mwa Asia walipokutana ili kupitia upya mpango wao wa kikanda wa amani uliokwama kwa Myanmar.

Umoja huo unakutana huku kizungumkuti kwa jeshi kikiongezeka kutokana na kushindwa kukomesha ghasia zaidi ya miaka miwili baada ya kunyakua mamlaka katika mapinduzi.

Waziri wa mambo ya nje wa Malaysia Zambry Abdul Kadir aliwaambia waandishi wa habari baada ya mazungumzo katika mji mkuu wa Indonesia kwamba, hawawezi kuruhusu hali hiyo kuendelea, nchini Myanmar.

"Malaysia na nchi nyingine wanachama hatuwezi kuruhusu hili kuendelea bila hatua kali na madhubuti zilizowekwa kwa serikali ya kijeshi."

Hakuwataja wanachama wengine wa Jumuiya ya Mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia (ASEAN) ambao walitoa mitazamo wao kuhusu jambo hilo.

ASEAN Kusaka suluhu ya amani ya Myanmar 

Viongozi wa ASEAN wanakutana mjini Jakarta wiki hii kuijadili Myanmar, kanuni ya maadili ya Bahari ya Kusini ya China, uchumi wa kanda hiyo, uhalifu wa kimataifa na masuala mengine.

Waziri wa Mambo ya Njea Malaysia Zambry Abdul Kadir kushoto, akiwa na mwenzake wa Singapor Vivian Balakrishnan.Picha: Mast Irham/AP Photo/picture alliance

Myanmar ni mwanachama wa ASEAN ingawa watawala wake wa kijeshi wameondolewa kwenye mikutano ya jumuiya hiyo tangu walipoitoa serikali ya kidemocrasia ilioongozwa na Aung San Suu Kyi mnamo 2021, ikichochea upinzani mkali kwa utawala wao.

ASEAN imekubaliana juu ya mpango wa amani, unaojulikana kama makubaliano yake yenye vipengele vitano, ambayo yanataka kukomesha ghasia na kufanyika mazungumzo kati ya vyama vyote, lakini majenerali hawajazingatia kwa umakini mpango huo.

Zambry alisema mpango wa amani haujatekelezwa ipasavyo kwa sababu ya "vikwazo vilivyowekwa na utawala wa kijeshi".

Msemaji wa jeshi la serikali ya Myanmar hakupatikana mara moja kuzungumzia hoja hiyo lakini viongozi wa kijeshi wamekuwa wakipinga ukosoaji kutoka nje ya nchi wakisema wanajukumu la kutetea nchi dhidi ya maadui.

Kwanini ASEAN inakigugumizi kuamua?

Ghasia nchini Myanmar zimeibua maswali kuhusu ufanisi na umoja wa jumuia ya kisiasa ya ASEAN, ilioanzishwa kwenye kilele cha Vita Baridi katika miaka ya 1960 kupinga kuenea kwa ukomunisti.

UN: Mauaji bado yanaendelea Myanmar

01:06

This browser does not support the video element.

Kwa miaka mingi ASEAN iliendeleza "mazungumzo yenye kujenga" na jeshi la Myanmar, licha ya shinikizo la mataifa ya Magharibi kuwatenga majenerali waliotawala kwa muda mrefu na kuwashinikiza kufanyika kwa mageuzi kupitia vikwazo. 

Mapinduzi ya mapema ya 2021 yalimaliza muongo mmoja wa mageuzi ya muda, ikiwa ni pamoja na chaguzi mbili alizoshinda mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Suu Kyi, na kurudisha nyuma matumaini katika ASEAN na kwingineko kwamba, Myanmar ilikuwa inaelekea kwenye serikali ya kiraia, utulivu wa kisiasa na ukuaji wa uchumi.

ASEAN kwa miongo kadhaa imekuwa ikifanya kazi chini ya kanuni ya kutoingilia masuala ya ndani ya kila nchi mwanachama na kufikia makubaliano kwa mazungumzo.

Hun Manet waziri mkuu mpya wa Kambodia, alisema jumuiya hiyo lazima izuie matumizi ya nguvu dhidi ya mataifa huru katika ulimwengu unaozidi kuwa hatari.

"Tunaishi katika wakati mgumu na kutokuwa na uhakika mkubwa,"

aliongeza kwamba ushindani wa kutanua ushawishi wa kisiasa kati ya mataifa makubwa unazidi kuongezeka, na kusababisha mabadiliko ya mara kwa mara katika uchumi wa kikanda na kimataifa na biashara.

"Hii inaweka shinikizo kubwa kwa amani, usalama na ustawi kwa ASEAN kwa ujumla." Hun Manet alisisitiza.

Indonesia, ambayo imehimiza umoja huku kukiwa na mashaka yanayoongezeka juu ya uaminifu wa umoja huo, imekuwa ikifanya juhudi za nyuma ya pazia kutafuta suluhu la machafuko ya Myanmar lakini haina mengi ya kuonyesha katika juhudi zake.

Nchi washirika kuhuduria mkutano huo

Baadae wiki hii viongozi na maafisa wa ngazi ya juu kutoka nchi washirika  wa jumuiya hiyo ikiwemo Marekani, China, Japan, Korea Kusini Australia na wengine watahudhuria mkutano huo utakaofanyika mjini Jakarta.

Mwaziri wa mambo ya Nje Marekani Antony Blinken, Korea kusini Park Jin na Japan Yoshimasa Hayashi.Picha: Dita Alangkara/Pool/REUTERS

Rais wa Marekani Joe Biden hatahudhuria mkutano huo, badala yake Makamu wa Rais Kamala Harris, makamu wa rais wa kwanza wa Marekani mwenye asili ya Asia, watamuawakilisha.

Waziri Mkuu wa China Li Qiang anatarajiwa kuhudhuria.